QATAR

Ndege za Qatar ruksa kwenda Misri

Shirika la ndege la Qatar
Shirika la ndege la Qatar PASCAL PAVANI / AFP

Misri inatarajia kufungua tena anga yake kwa ndege za Qatar Jumanne wiki hii na kuruhusu safari za ndege kuanza tena kati ya nchi hizo mbili, vyanzo kutoka uwanja wa ndege na vyombo vya habari vya serikali vimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unafuatia makubaliano, yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu, juu ya kuondolewa kwa zuio lililowekewa Qatar na Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri mnamo mwezi Juni 2017.

Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Bahrain tayari wametangaza kufungua tena anga zao kwa ndege kutoka Qatar.

Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri zilikuwa zimekata uhusiano wote wa kidiplomasia na Qatar mnamo Juni 5, 2017 kwa tuhuma ya kwamba "Qatar inasaidia vikundi vya kigaidi" na kuanza kuweka vizuizi cha kiuchumi kwa nchi hii.

Huku Qatar ikiwa imekana mashtaka yote ya nchi hizi, hali hii ilisababisha mgogoro katika eneo la Ghuba.