URUSI-SYRIA-MAREKANI-DIPLOMASIA

Moscow 'yalaani vikali' mashambulizi anga ya Marekani nchini Syria

Jeshi la Syria katika mkoa wa Allepo
Jeshi la Syria katika mkoa wa Allepo AFP

Urusi 'inalaani vikali' mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii Mashariki mwa Syria, Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi imesema Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

"Tunalaani vikali vitendo kama hivyo," msemaji wa wizara hiyo Maria Zakharova amesema. "Tunatoa wito kwa heshima isiyo na masharti kwa uhuru wa taifa la Syria."

Urusi imeingilia kijeshi nchini Urusi ikisaidia utawala wa Bashar al-Assad tangu 2015.

Kremlin imesema inafuatilia hali hiyo kwa karibu, ikiongeza kuwa haikubaliani na Marekani kuwa iliionya Urusi kabla ya kutekeleza mashambulizi hao, mawasiliano haya ya kiutendaji yanafanywa katika maeneo ya kivita kati ya jeshi.