Syria: Wapiganaji 17 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani

Ndege mbili za kivita za jeshi la majini la Marekani aina ya F-18E wakati wa operesheni ya kuongeza mafuta angani katika eneo la Mashariki ya Kati (picha ya kumbukumbu).
Ndege mbili za kivita za jeshi la majini la Marekani aina ya F-18E wakati wa operesheni ya kuongeza mafuta angani katika eneo la Mashariki ya Kati (picha ya kumbukumbu). © AFP

Jeshi la Marekani limeshambulia kambi zinazokaliwa na wapigani wa Iran wanaoungwa mkono na serikali ya Syria.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya ulinzi nchini Maarekani John Kirby kwenye taarifa kwa vyombo vya habari ,amesema mashambulizi hayo kutumia ndege za kijeshi yamefanyika kufuatia maelekezo ya rais Joe  Biden,lengo likiwa kujibu mashambulizi ya makombora ya waasi wa Syria kwenye kambi za wanajeshi wa Marekani, na kukabiliana na tishio la aina hilo.

Wizara ya ulinzi imesema mashambulizi hayo  ambayo wapiganaji wa kundi linalojiita Awliya al-Dam  au  the Guardians of the Blood wamekiri kuhusika ,yameharibu  miundo misingi  kadhaa ya jeshi la Marekani eneo la mpakani.

Aidha Marekani imesema mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi yamefanywa chini ya utararibu hitajika na kujumuisha mbinu za kidiplomasia baada ya makubaliano na washirika wake.

Makundi ya waasi ambayo yameonekana kuungwa mkono na Iran ni pamoja na Kataib Hezbollah na Kataib Sayyid al Shuhada.