PALESTINA-ISRAELI-ICC-HAKI

Mwendesha mashtaka wa ICC atangaza uchunguzi katika maeneo ya Wapalestina

Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda,
Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, ©ICC-CPI

Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda, ametangaza katika taarifa yake Jumatano kufungua uchunguzi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita uliofanywa katika maeneo ya Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Mnamo Februari 5, ICC iliamua kwamba mamlaka yake yaliongezeka hadi maeneo ya Wapalestina.

"Uamuzi wa kufungua uchunguzi unafuatia uchunguzi wa awali uliofanywa kwa uangalifu na Ofisi yangu kwa karibu miaka mitano," Fatou Bensouda amesema katika taarifa yake.

Mnamo mwezi Desemba 2019, mwanasheria mkuu wa ICC aliamua kuwa uhalifu wa kivita ulikuwa ukifanyika au ulikuwa ukifanywa katika Ukingo wa Magharibi, pamoja na Jerusalem Mashariki, na Ukanda wa Gaza. Ilikuwa imebaini kama wahusika wa uhalifu huo vikosi vya ulinzi vya Israeli na makundi yenye silaha ya Wapalestina kama Hamas.