IRAQ-VATICAN

Papa Francis aadhimisha misa ya kwanza ya kiuchungaji katika historia ya Iraq

Papa Francis aongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph la Walkadea huko Baghdad Machi 6, 2021.
Papa Francis aongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph la Walkadea huko Baghdad Machi 6, 2021. REUTERS - AHMED JADALLAH

Kiongozi wa kanisa Katoliki dunini Papa Francis anaendelea na ziara yake nchini Iraq na leo Jumapili anatarajia kzuru mji wa Mosul.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano wake wa kihistoria na kiongozi wa Waislamu wa madhebu ya Shia, Ayatollah Ali al Sistani kwenye mji mtakatifu wa Najaf, Kiongozi wa Kanisa Katoliki aliadhimisha Ibada ya Misa katika Kanisa Katoliki la Walkadea la Mtakatifu Joseph mjini Baghdad, Iraq.

Mkuu wa Kanisa Katoliki la Walkadea, Kadinali Louis Raphaeli I Sako, ameiita zira ya Papa Francis kama ''iliyopokelewa kwa furaha na Kanisa lote.''

Papa Francis awataka watu kuhurumiana

Papa Francis anakuwa kingozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki kuongoza Misa kwa kutumia liturjia ya Ibada ya Kanisa Katoliki la Mashariki. Papa Francis ametoa wito wa umoja na amani kati ya watu.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 84, amewaambia waumini kuwa sio matajiri na wenye nguvu ambao wamebarikiwa, ''bali wale wanaowahurumia ndugu zao.''

Pia alilizuru eneo linaloaminika kuwa sehemu ya kuzaliwa Abrahamu. Leo Papa Francis anatarajiwa kuizuru Mosul ambayo ilikuwa ngome kuu ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.