Papa Francis katika siku ya mwisho ya ziara yake Iraq

Pope Francis, akitazama majengo ya kanisa ambayo yaliharibiwa na wapiganaji wa IS nchini Iraq, 7 March 2021.
Pope Francis, akitazama majengo ya kanisa ambayo yaliharibiwa na wapiganaji wa IS nchini Iraq, 7 March 2021. AP - Andrew Medichini

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, ametembelea eneo la kaskazini mwa nchi ya Iraq, ambako wakati fulani lilikaliwa na wapiganaji wa Islamic State, hii ikiwa ni katika siku yake ya tatu na ya mwisho ya ziara yake nchini Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Waumini wa Kikristo ni miongoni mwa waliolengwa na kundi la IS wakati walipovamia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2014, maeneo ambayo kwa sehemu kubwa yanakaliwa na wakristo walio wachache nchini humo, ambapo walitekeleza vitendo vingi vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Papa Francis aliwasili kwenye mji wa Mosul na kufanya ibada katika moja ya makanisa yaliyoharibiwa na wapiganaji wa IS.

Baadae alifanya ibada maalumu katika mji wa Irbil, ambapo watu zaidi ya elfu 10 walitarajiwa kuhudhuria.

Hata hivyo kumekuwa na hofu kuwa huenda ibada yake ikawa ni sehemu ya kueneza maambukizi ya virusi vya Corona, ambavyo nchi hiyo bado inakabiliana navyo.

Iraq imeshuhidia ongezeko la maambukizi ya Covid 19 katika mwezi mmoja uliopita, lakini Papa Francis na timu yake wote walikuwa wamepewa chanjo ya Covid 19, huku Iraq ikiwa imepokea chanjo ya kwanza juma lililopita.

Ziara ya Papa inatoa matumaini kwa wakristo

Ziara hii ya siku 4 ambayo ilianza siku ya Ijumaa, ni ya kwanza kufanywa na Papa Francis nje ya Italia tangu kuripotiwa kwa mara ya kwanza kwa maambukizi ya virusi vya Corona duniani mwaka mmoja uliopita, na hii ikiwa ni ziara ya kwanza ya Papa kwenye taofa hilo.

 

Afisa wa polisi akiwa amesimama kando ya pango lenye picha ya Papa Francis mjini Baghdad Iraq, Ijumaa, March 5, 2021. Pope Francis heads to Iraq on Friday to urge the country's dwindling number of Christians to stay put and help rebuild the country after years of war and persecution, brushing aside the coronavirus pandemic and security concerns. (AP Photo/Andrew Medichini)
Afisa wa polisi akiwa amesimama kando ya pango lenye picha ya Papa Francis mjini Baghdad Iraq, Ijumaa, March 5, 2021. Pope Francis heads to Iraq on Friday to urge the country's dwindling number of Christians to stay put and help rebuild the country after years of war and persecution, brushing aside the coronavirus pandemic and security concerns. (AP Photo/Andrew Medichini) AP - Andrew Medichini

Papa alienda wapi na wapi siku ya Jumapili?

Baada ya kuwasili Irbil, alipokelewa na kiongozi wa eneo la mkoa wa Kurdistan, Nechirvan Barzani.

Baadae alisafiri kwa kutumia ndege hadi Mosul ambapoko alitembelea kanisa la kihistoria na kufanya maombi na wahanga wa vitendo vya IS, ambapo maelfu waliuawa katika vita dhidi ya kundi hilo.

Akiwa amezingirwa na maeneo yaliyoharibika ya kanisa, papa Francis alisema;

Wakristo kutoka Iraq na mashariki ya kati, hawajawahi kufanya makosa kwa mtu wala jamii zinazo wazunguka na hata kwa jamii walizoziacha nyuma.

Ni ujumbe gani ambao Papa anautoa?

Tangu awasili mjini Baghdad siku ya Ijumaa, Papa Francis ametoa wito wa kumalizika kwa machafuko na uenezi wa itikadi kali ambapo amesema, Wakristo walioko Iraq wanapaswa kutoa mchango mkubwa kama wananchi, kwa uhuru na kwa uwajibikaji.