SYRIA

Bashar al Assad na mkewe wakutwa na virusi vya Corona

vikosi vya jeshi la Syria, Katibu mkuu wa chama tawala cha Ba’ath na Katibu wa Kanda wa tawi la chama hicho nchini Syria.
vikosi vya jeshi la Syria, Katibu mkuu wa chama tawala cha Ba’ath na Katibu wa Kanda wa tawi la chama hicho nchini Syria. SANA/AFP

Rais wa Syria Bashar al Assad na mkewe Asma wameambukizwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, ikulu ya rais nchini Syria imetangaza leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Bashar na Asma al-Assad wamefanya vipi,o vya Corona baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo na matokeo yake ni kwa,ba wamea,bukizwa virusi hivyo, ikulu imeongeza.

Hata hivyo wote wawili wanaendelea vizuri na wataendelea kutekeleza majukumu yao; huku wakijiweka karantini  kwenye makazi, kulingana na ikulu ya rais nchini Syria.

Bashar Hafez al-Assad ndiye rais wa Syria, Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya jeshi la Syria, Katibu mkuu wa chama tawala cha Ba’ath na Katibu wa Kanda wa tawi la chama hicho nchini Syria.

Julai 10, 2000 Assad alichaguliwa kuwa rais, akimrithi baba yake Hafez Assad, alieiongoza Syria kwa miaka 30.