SYRIA

Miaka 10 tangu kuzuka kwa maandamano ya amani yaliogeuka kuwa vita nchini Syria

Askari wa Syria akipita karibu na picha za Vladimir Putin na Bashar al-Assad, mashariki mwa Ghouta (Damescus), Februari 28, 2018.
Askari wa Syria akipita karibu na picha za Vladimir Putin na Bashar al-Assad, mashariki mwa Ghouta (Damescus), Februari 28, 2018. REUTERS/Omar Sanadiki

Raia wa Syria wanatimiza miaka 10 tangu kuzuka kwa maandamano ya amani kumwondoa madarakani rais Bashar Assad na serikali yake. 

Matangazo ya kibiashara

Licha ya mapigano ya mwongo mmoja, ambayo yamesababisha maafa makubwa na mamilioni ya raia wa Syria kuyakimbia makwao, rais Assda amesalia madarakani. 

Kuendelea kwake kuwa uongozini, kunatokana na usaidizi mkubwa wa kijeshi kutoka nchini Iran na Urusi, mataifa ambayo yameendelea kusisimama na rais Assad katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati. 

Syria imeharibiwa mno kutokana na vita vinavyoendelea, na karibu watu Laki tano wameauwa huku wengine zaidia ya Milioni 20 wakisalia bila makaazi na Milioni tano wamekimbilia katika mataifa jirani. 

Mamilioni ya wananchi wa Syria, wameendelea kuwa masikini, wakati huu makundi yenye silaha yakiendelea kudhibiti mkoa wa Idlib kwa usaidisi wa waasi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki.

Miaka 10 ya vita, rais Assad akiendelea kuwa madarakani, Umoja wa Mataifa unasema kuwa asilimia 80 ya raia wa Syria wanaishi kwa umasikini mkubwa, na asilimia 60 wapo kwenye hatari kubwa ya kukabiliwa na baa la njaa.