AFGHANISTANI

Afghanistan: Wanne wauawa katika mlipuko wa gari la serikali Kabul

Maafisa wa Afghanistan wanakagua basi dogo lililoharibika vibaya baada ya mlipuko huko Kabul, Afghanistan Machi 15, 2021.
Maafisa wa Afghanistan wanakagua basi dogo lililoharibika vibaya baada ya mlipuko huko Kabul, Afghanistan Machi 15, 2021. REUTERS - MOHAMMAD ISMAIL

Watu wanne wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa leo Alhamisi wakati gari lililokuwa limebeba wafanyakazi wa serikali lilipokanyaga kilipuzi huko Kabul, nchini Afghanistan, mamlaka imesema.

Matangazo ya kibiashara

Basi lililokuwa limebeba wafanyakazi wa Wizara ya Habari na Teknolojia limekanya kifaa cha kulipuka kilichowekwa kando ya barabara, amesema Abdul Samad Hamid Poya, mshauri wa wizara hiyo.

Hakuna kundi ambalo limedai shambulio hilo, lakini kundi la Taliban hivi karibuni lilitekelewa mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa serikali, viongozi wa mashirika ya kiraia na waandishi wa habari, kulingana na mamlaka nchini Afghanistan imesema. Taliban, hata hivyo, wamekanusha madai hayo.

Mlipuko huu unatokea siku ambayo kunafanyika mkutano huko Moscow ambao wawakilishi wa Afghanistan, Taliban na nchi kadhaa, pamoja na Mareani wanashiriki, kwa lengo la kupunguza machafuko nchini Afghanistan ili kuendeleza mchakato wa amani.

Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan pia imesema leo Alhamisi kwamba wanajeshi tisa wameuawa katika ajali ya helikopta Jumatano jioni.