MAREKANI

Utawala wa Biden wataka kurejesha uhusiano na Palestina

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas. REUTERS

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden unajikita na mpango wa kuanzisha tena uhusiano kati ya Washington na Palestina, ambao ulizorota kabisa wakati wa muhula wa Donald Trump, rasimu ya kumbukumbu ya ndani inaonyesha.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo viwili vilivyo na taarifa kuhusu hati hiyo iliyoandikwa na wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Umoja wa Falme za Kiarabu The National, vimesema bado ni rasimu kwa wakati huu, lakini hiyo -inaweza kusaidia kwa baadaye kurejelea mambo kadhaa ya sera iliyotekelezwa na Donald Trump, ambayo Wapalestina walishutumu kuwa ni nzuri kwa Israeli.

Tangu kuapishwa kwa Joe Biden Januari 20, washauri wake wameashiria nia ya rais wa Marekani kufufua tena uhusiano na Palestina.

Utawala mpya umeahidi kurejesha mamia ya mamilioni ya dola katika misaada ya kiuchumi na kibinadamu na kufanya kazi ya kufungua tena ujumbe wa kidiplomasia wa Palestina nchini Marekani.

Washauri wa Joe Biden pia wameelezea wazi nia ya kuanzisha tena kama kipaumbele cha Marekani mpango wa suluhisho la nchi mbili kumaliza mzozo kati ya Israeli na Palestina. Lakini wanaendelea kwa uangalifu wakati uchaguzi wa wabunge

unakaribia nchini Israeli Machi 23 na uchaguzi wa Palestina umepangwa kufanyika baadaye mwaka huu.