YEMENI

Saudi Arabia yataka waasi wa Houthi kusitisha mapigano

SMapigano yanaendelea kurindima kati ya vikosi vya serikali na waaasi wa Houthi Yemeni.
SMapigano yanaendelea kurindima kati ya vikosi vya serikali na waaasi wa Houthi Yemeni. - AFP/File

Saudi Arabia imependekeza kusitishwa kwa mapigano "kamili" ili kumaliza mzozo mkubwa nchini Yemen, ambao umehusisha waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya vikosi vya serikali, vikisaidiwa na muungano unaoongozwa na Riyadh. Waasi wa Houthi wamefutilia mbali pendekezo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia, ambayo imeingilia kijeshi nchini Yemen tangu mwaka 2015, imetoa mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na "kusitisha mapigano kamili nchini kote chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa," serikali ya Saudi ilisema katika taarifa.

Riyadh pia imependekeza uwanja wa ndege wa mjini Sana'a, mji mkuu wa Yemen ulioshikiliwa na waasi ufunguliwe, na kuzindua tena mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali ya Yemen na Wahouthi, imeongezwa katika taarifa.

Waasi hao walikuwa wamefungua hivi karibuni nafasi zote za anga na baharini nchini Yemen, chini ya udhibiti wa Saudia, sharti muhimu kwa mchakato wa mazungumzo.

"Tunataka kusitishwa kwa mapigano," Waziri wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Faisal ben Farhane amewaambia waandishi wa habari katika mkutano huko Riyadh. "Mpango huo utatekelezwa mara tu Wahouti watakapoukubali," ameongeza.