ISRAELI

Israeli: Benjamin Netanyahu apata ushindi mdogo katika uchaguzi wa wabunge

Wafuasi wa Benjamin Netanyahu waonyesha furaha yao baada ya kupiga kura katika makao makuu ya chama cha Likud huko Jerusalem Machi 24, 2021.
Wafuasi wa Benjamin Netanyahu waonyesha furaha yao baada ya kupiga kura katika makao makuu ya chama cha Likud huko Jerusalem Machi 24, 2021. REUTERS - RONEN ZVULUN

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini Israel yanaonesha kuwa kwa mara nyingine, hakuna mshindi wa moja kwa moja kuunda serikali baada ya wananchi wa taifa hilo kupiga kura hapo jana.

Matangazo ya kibiashara

Duru zinasema kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kwa mara nyingine atashindwa kupata ushindi unaohitajika kuunda serikali, licha ya chama chake cha Likud kuonekana kuongoza.

Hii ni mara nne kwa Netanyahu kushindwa kupata ushindi wa kumwezesha kupata ushindi wa moja kwa moja, baada ya uchaguzi wa nne ndani ya miaka miwili.

Inatarajiwa kuwa, chama cha Netanyahu kinatarajiwa kupata ushindi kwa kupata viti 52 au 53 kati ya 120 vinavyowaniwa, na wapinzani wake wanatarajiwa kupata viti 60 ikiwa ni ishara kuwa Netanyahu hawezi kupata ushindi unaohitajika.

Matokeo ya mwisho huenda yakachukua siku kadhaa kabla ya kufahamika, na hali ikiendelea kuwa hivi, nchi hiyo italazimika kushiriki kwenye uchaguzi wa tano kupata chama au miungano utakaopata ushindi unaohitajika ikuunda serikali.

Hata hivyo, atakayeunda serikali atalazimika kushirikiana na Naftali Bennett kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia Yamina, anayetarajiwa kupaya viti saaba au nane.