UN-SAUDIA

UN: Mchunguzi wetu alitishiwa na Riyadh katika kesi ya Khashoggi

Agnes Callamard, mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yanayotekelezwa na maafisa wa serikali, akizungumza na Hatice Cengiz, aliye kuwa mchumba wa mwandishi wa habari aliyeuawa Jamal Khashoggi, huko Brussels, Ubelgiji Desemba 3, 2019.
Agnes Callamard, mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yanayotekelezwa na maafisa wa serikali, akizungumza na Hatice Cengiz, aliye kuwa mchumba wa mwandishi wa habari aliyeuawa Jamal Khashoggi, huko Brussels, Ubelgiji Desemba 3, 2019. REUTERS - Francois Lenoir

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imethibitisha ukweli wa taarifa zilizochapishwa na Gazeti la The Guardian la Uingereza, ambapo mtaalam anayesimamia uchunguzi wa mauaji ya Jamal Khashoggi anasema alifanyiwa vitisho na mwakilishi mwandamizi wa Saudia.

Matangazo ya kibiashara

Katika maneno yaliyochapishwa Jumanne na Gazeti la The Guardian, Agnes Callamard, mchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binaadamu kuhusu mauaji yanayotekelezwa na maafisa wa serikali, alisema alionywa kuwa afisa wa Saudia alitishia "kumshughulikia" ikiwa ataendelea na uchunguzi juu ya mauaji ya Jamal Khashoggi.

Mamlaka nchini Saudi Arabia haijazungumza chochote kuhusiana na madai hayo. Akihojiwa na shirika la habari la REUTERS, Agnes Callamard hakutaka kutoa maelezo zaidi kuhusiana na vitisho hivyo.

"Tunathibitisha kuwa maelezo katika nakala ya Gazeti la The Guardian juu ya tishio dhidi ya Agnes Callamard ni ya kweli," msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Rupert Colville amesema katika barua pepe, akijibu shirika la habari la REUTERS.