AFGHANISTANI

Taliban kuanza tena mashambulizi dhidi ya Wamarekani

Mjumbe wa amani kutoka Marekani Zalmay Khalilzad, kushoto, na Mullah Abdul Ghani Baradar, kiongozi mkuu wa kisiasa wa kundi la Taliban, wanasaini mkataba wa amani kati ya Taliban na Marekani.
Mjumbe wa amani kutoka Marekani Zalmay Khalilzad, kushoto, na Mullah Abdul Ghani Baradar, kiongozi mkuu wa kisiasa wa kundi la Taliban, wanasaini mkataba wa amani kati ya Taliban na Marekani. AP - Hussein Sayed

Kundi la Taliban limetishia kuanza tena mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ikiwa hawataondoka nchini humo kwa tarehe iliyopangwa Mei 1.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, rais wa Marekani Joe Biden alisema itakuwa vigumu kwa jeshi la Marekani kuheshimu tarehe ya mwisho iliyokubaliwa mwaka jana kati ya waasi na Washington.

Katika taarifa, Taliban wamesema "watalazimika kuendelea na jihadi yao na mapambano yao ya silaha dhidi ya vikosi vya kigeni kuikomboa nchi yao" ikiwa tarehe ya Mei 1 haitazingatiwa.