AFGHANISTANI

Afghanistan: Mkutano wa kuendeleza mchakato wa amani waandaliwa Istanbul

Mjumbe wa Marekani kwa Afghanistan na Pakistan Zalmay Khalilzad huko Kabul Machi 9, 2020.
Mjumbe wa Marekani kwa Afghanistan na Pakistan Zalmay Khalilzad huko Kabul Machi 9, 2020. © AP - Rahmat Gul

Baada ya Moscow, mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya amani nchini Afghanistan Zalmay Khalilzad alikuwa Uturuki Jumamosi hii, Machi 27, kuendelea na ziara yake ili kuendeleza mazungumzo ya amani nchini Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Uturuki itakuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu mchakato wa amani nchini Afghanistan mapema mwezi Aprili na inatarajia kutoa msukumo mpya kwa mazungumzo hayo.

Baada ya Moscow, ni zamu sasa ya Istanbul. Mkutano ujao nchini Uturuki kuhusu amani nchini Afghanistan unaonekana kama fursa ya kupumua ya kutoa mwelekeo mpya katika mazungumzo ya amani kati ya mamlaka ya Afghanistan na Taliban.

Uturuki, mwanachama wa NATO na mshirika wa kiuchumi wa Afghanistan, inatarajia kuchukua jukumu katika kuharakisha mazungumzo, ambayo yamekuwa magumu tangu yalipoanza mwezi Septemba mwaka uliyopita. Na kuna uharaka. Kwa sababu zimebaki wiki 5 tu kabla ya tarehe ya mwisho, Mei 1.

Marekani imeahidi kuondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan ifikapo Mei 1 kama sehemu ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Taliban Februari 29, 2020 huko Doha, nchini Qatar. Wakati huo huo Taliban iliahidi kuacha kushambulia wanajeshi wa Marekani na wale wa NATO na kushiriki mazungumzo ya amani kati ya wadau wote nchini Afghanistan. Lakini mazungumzo yamekwama.

Wanajeshi 9,600 wa kigeni nchini Afghanistan

Lakini Merika bado haijaamua ikiwa itabakiza wanajeshi wake au kuwaondoa nchini Afghanistani, kama unavyosema mkatab huo. Kwa upande wake Taliban ilionya siku ya Ijumaa (Machi 26) kwamba itaanzisha tena mapigano na vikosi vya kigeni ikiwa wataamua kubaki nchini humo baada ya tarehe hiyo.

Kuna vikosi 9,600 vya kigeni vilivyobaki nchini Afghanistan. Kati yao, 2,500 ni Wamarekani. Wakati hakuna mashambulio yoyote yaliyoelekezwa dhidi ya vikosi vya kigeni tangu makubaliano ya Doha, mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali na wafanyakazi yameongezeka.