YEMENI

Waasi wa Houthis nchini Yemen wadai kushambulia mji mkuu wa Saudia

Waasi wa Houthi, Januari 2021 (picha ya kumbukumbu).
Waasi wa Houthi, Januari 2021 (picha ya kumbukumbu). REUTERS - KHALED ABDULLAH

Msemaji wa waasi wa Kishia wa Houthi wa Yemen amesema siku ya Alhamisi kwamba kundi hilo limeshambulia kwa msaada wa ndege wanne zisizo na rubani mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh. Mamlaka ya Saudia haijathibitisha shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Houthis, walio na mafungamano na Iran, walifutilia mbali pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Riyadh mwezi mmoja uliopita kwa sababu haikuondoa kizuizi cha angani na baharini kilichowekwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika maeneo wanayodhibiti hasa kaskazini mwa Yemen.

Mzozo huo, unaochukuliwa katika ukanda huo kama vita kati ya Saudi Arabia na Iran, ndio sababu kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kunaendelea kuriotiwa mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.