JORDAN

Jordan: Mwana Mfalme Hamzah ahusishwa katika jaribio la mapinduzi

Mfalme wa Jordan Abdullah II ahutubia Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Ufaransa Januari 15, 2020
Mfalme wa Jordan Abdullah II ahutubia Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Ufaransa Januari 15, 2020 © Vincent Kessler/REUTERS

Jordan imesema imefakiwa kuzuia jaribio la mapinduzi dhidi ya uongozi wa Kifalme lililomhusisha kaka wa Mfalme Abdulah wa pili.

Matangazo ya kibiashara

Watu 16 wamekamatwa kufuatia jaribio hilo na wanadaiwa kushirikiana na watu wa kigeni kujaribu kumwondoa madarakani Mfalme Abdullah.

Mshukiwa Mkuu ni aliyekuwa Mwana Mflame Hamzah bin Hussein aliyeondolewa katika nafasi hiyo mwaka 2004. Anadaiwa kutishia usalama wa Kifalme.

Mana Mfalme Hamza bin Hussein akitoa hotuba kwa maulama wa Kiislamu na wasomi katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kidini katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al al-Bayet huko Amman
Mana Mfalme Hamza bin Hussein akitoa hotuba kwa maulama wa Kiislamu na wasomi katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kidini katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al al-Bayet huko Amman REUTERS - REUTERS PHOTOGRAPHER

Hata hivyo Malkia Nour wa Jordan ambaye ni mama wa mrithi wa zamani wa ufalme, Mwana Mfalme Hamzah al-Hussein, amesema madai yanayomkabili mwanawe kwamba alihusika katika vitendo vya kutatiza usalama nchini humo, ni fitina ya kumuharibia jina tu. Nour, ambaye ni mama wa kambu wa mfalme wa sasa wa Jordan, Abdullah wa Pili, alisema katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa Twitter, kwamba anaomba "ukweli na haki ujitokeze kwa wale wote waliochafuliwa jina."

Mwanafalme Faisal bin Farhan Al Saud ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, ameimbia France 24 kuwa Saudi Arabia inaunga mkono hatua zilizochukuliwa na mshirika wake Jordan.