PALESTINA

Washington yarejesha msaada kwa Wapalestina, Israeli yapinga

Marekani itasaidia tena kufadhili UNRWA kwa  kiwango cha dola Milioni 150.
Marekani itasaidia tena kufadhili UNRWA kwa kiwango cha dola Milioni 150. AFP

Marekani imetangaza kuanza tena kutoa msaada kwa Wapalestina, uliositishwa chini ya tawala wa Donald Trump, uamuzi uliopingwa mara moja na balozi wa Israeli mjini Washington, na kupongezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa Wakimbizi  wa Palestina ( UNWRA).

Matangazo ya kibiashara

Msaada huu kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa Wakimbizi  wa Palestina utafikia dola milioni 235. Marekani itachangia tena ufadhili wa shirika hili la Umoja wa Mataifa kwa dola milioni 150. Washington pia itachangia dola milioni 75 kwa maendeleo na uchumi wa Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, na dola milioni 10 kwa mchakato wa amani.

"Msaada wa Marekani kwa raia wa Palestina hutokana na masilahi na maadili ya Marekani. Marekani itanoa msaada muhimu kwa wale wanaohitaji, inakuza maendeleo ya kiuchumi na inasaidia mazungumzo ya Israeli na Palestina, uratibu wa usalama na utulivu, "Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema katika taarifa.

Hata hivyo Israel ambayo imechukua msimamo wa kuukosoa utawala wa  Biden imesema kurejeshwa msaada  kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa huduma ya maakazi, elimu na usaidizi mwingine kwa zaidi ya wakimbizi wa kipalestina milioni 6 ni jambo la fedheha.