YEMENI

Yemen: Mapigano yaongezeka Marib, licha ya wito wa kusitishwa vita

Mwanajeshi wa serikali akitoa ulinzi katika ngome dhidi ya waasi wa Houthi katika jimbo la Marib, Aprili 6, 2021.
Mwanajeshi wa serikali akitoa ulinzi katika ngome dhidi ya waasi wa Houthi katika jimbo la Marib, Aprili 6, 2021. STR AFP

Mapigano kati ya waasi wa Houthi na vikosi vya vinavyotii serikali katika eneo la Marib, ngome ya mwisho inayoshikiliwa na vikosi vya serikali nchini Yemen, yamesababisha  vifo vya watu 53 katika kipindi cha saa 24 zilizopita kwa pande zote mbili.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hii ya vifo imetolewa  na jeshi la serikali, lakini haijathibitishwa na waasi wa Houthi.

Wanajeshi 22 kwa upande wa vikosi vya serikali, pamoja na maafisa watano, na 31 katika safu ya waasi. Waasi wa Houthi hutangaza mara chache hasara kwa upande wao.

Mapigano yalikuwa mali katika maeneo ya kivita ya Kassara na Machjaa, kaskazini magharibi mwa Marib, mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta. Waasi wamekuwa wakijaribu tangu mwanzoni mwa Februari kuteka ngome hii ya vikosi vya serikali, iliyoko kilomita 120 kutoka mji mkuu Sanaa, unaodhibitiwa na waasi wa Houthi tangu mwaka 2014, kama sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi.