IRAN

Iran yasitisha "ushirikiano" wake na nchi za EU katika sekta kadhaa

Rais wa Iran Hassan Rouhani.
Rais wa Iran Hassan Rouhani. - Iranian Presidency/AFP

Tehran imetangaza tangu jana Jumatatu Aprili 12, kusitisha ushirikiano wake katika sekta kadhaa na  Umoja wa Ulaya, saa chache baada ya EU kuchukuwa vikwazo dhidi ya maafisa wanane wa usalama wa Iran kwa jukumu lao katika ukandamizaji mkubwa wa maandamano nchini humo mwezi Novemba 2019.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya uliamua kuongeza hadi Aprili 13, 2022 hatua za vizuizi zilizowekwa tangu 2011 kujibu visa vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Iran, na Jumatatu wiki hii umoja huo uliongeza watu wanane na idara tatatu kwenye orodha hii ya vikwazo kwa sababu ya jukumu lao katika kukandamiza maandamano mwezi Novemba 2019 nchini Iran.

Orodha hiyo sasa inajumuisha jumla ya watu 89 na idara 4. Wanane wapya walioidhinishwa ni makamanda wa wanamgambo wa Iran, polisi na vikosi maalum na mkurugenzi wa zamani wa gereza la Evin. Idara hizo tatatu ni magereza ya Evin, Fashafouyeh na Rajaee Shah.

Vikwazo vinajumuisha marufuku ya kusafiri na kuzuia mali zao. Umoja wa Ulaya pia umepiga marufuku usafirishaji wa vifaa vinavyoweza kutumiwa kwa ukandamizaji wa ndani na vifaa vya uchunguzi wa mawasiliano ya simu nchini Iran. Kwa kuongezea, raia na makampuni ya Umoja huo ni marufuku kutoa pesa kwa kuwapa watu na taasisi zilizoorodheshwa.