MAREKANI

Wanajeshi 500 wa Marekani kuondoka Afghanistan Septemba 11

Askari wa Marekani akilinda kituo cha jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Logar.
Askari wa Marekani akilinda kituo cha jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Logar. REUTERS - Omar Sobhani

Rais wa Marekani Joe Biden, anatarajiwa kutangaza kuondoka kwa wanajeshi wa nchi hiyo wanaosalia nchini Afganistan, ifikapo tarehe 11 mwezi Septemba.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya Marekani hata hivyo, itakuja kwa kuchelewa kinyume na makubaliano ya serikali iliyopita, chini ya utawala wa Donald Trump ambaye alidhamiria wanajeshi hao 2500 wawe wameondoka nchini Afganistran ifikapo mwezi Mei.

Makataa haya mapya, yatakwenda sambamba na miaka 20 baada ya Marekani kushuhudia shambulizi la kigaidi katika majengo ya World Trade Center na Pentangon tarehe 11 Septemba mwaka 2001.

Rais Biden awali, alikuwa amedokeza kuwa kuondoka kwa wanajeshi hao kufikia tarehe 1 mwezi Mei, isingewezekana kwa sababu ingeweka hatarini maisha ya wanajeshi wa Marekani.

Licha ya kuwepo kwa mpango huu wa wanajeshi wa Marekani kuondoka, kundi la Taliban limeendelea kushtumiwa kwa kushindwa kuacha mashambulizi dhidi ya serikali ya Afganistan lakini pia vikosi vya Marekani.