IRAN

Afghanistan: NATO kuondoka Afghanistan sambamba na wanajeshi wa Marekani

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika Makao Makuu ya NATO, Machi 23, 2021.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika Makao Makuu ya NATO, Machi 23, 2021. © AFP

Wanajeshi wa kigeni waliopelekwa Afghanistan chini ya amri ya NATO wataondoka nchini humo kwa ushirikiano na wanajeshi wa Marekani, wanachama wa Transatlantic Alliance walikubaliana Jumatano, wakati rais wa Marekani Joe Biden alitangaza kujiondoa kwa Marekani nchini humo ifikapo Septemba 11.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wanajeshi 7,000 wasio wa Marekani sasa wako Afghanistan, ikiwa ni wanajeshi hasa kutoka nchi za NATO lakini pia kutoka Australia na New Zealand, wakati kikosi cha Marekani kikiwa na askari 2,500.

Vikosi vya NATO hutegemea Marekani hasa kwa msaada wa vyombo vya anga na kwa usimamizi wa mafunzo ya vikosi vya usalama vya Afghanistan.

Akiongea pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mkuu wa Pentagon Lloyd Austin ambao walikuwa ziarani Brussels, katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) amesema uamuzi huo ulikuwa shingo upande.

"Sio uamuzi rahisi, na kuna hatari inayoweza kutokea kufuatia uamuzi huo. Kama nilivyosema kwa miezi kadhaa, tunakabiliwa na shida. Kwa sababu njia mbadala ya kuondoka kwa utaratibu ni kujiandaa kwa ushiriki wa kijeshi wa muda mrefu na kipaumbele zaidi ni kwa wanajeshi zaidi wa NATO , "Jens Stoltenberg alisema katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya NATO.