MAREKANI

Joe Biden: Wanajeshi wa Marekani wataondoka Afghanistan Septemba 11

Joe Biden akizungumza kutoka Ikulu ya White House kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Aprili 14, 2021.
Joe Biden akizungumza kutoka Ikulu ya White House kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Aprili 14, 2021. AP - Andrew Harnik

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba wanajeshi wa Marekaniwatandoka nchini Afghanistan Septemba 11 badala ya Mei mosi kama alivyotangaza mtangulizi wake Donald Truamp.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotua yake kwa taifa Joe Biden amepongeza waajeshi hao, huku akidai kuwa "wametimiza lengo" lao nchini Afghanistan.

Rais Joe Biden ameahidi kwamba kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ifikapo Septemba 11 "hakutaharakishwa", na amewataka wapiganaji wa Taliban kukutekeleza "ahadi yao" kwa kutoitishia Marekani.

"Nadhani uwepo wetu nchini Afghanistan unapaswa kuzingatia kwa nini tulienda huko kwanza: kuhakikisha kwamba Afghanistan haitowi nafasi kwa makundi yenye itikadi kali kushambulia nchi yetu tena. Ndivyo tulivyofanya. Tumefanikisha lengo hili," amesema Rais Joe Biden.

NATO kuwaondoa wanajeshi wake Afghanistan

"Marekani itaanza itaanza kuondoa wanajeshi wake Mei 1," lakini "zoezi hilo halitaharakishwa," ameongeza Joe Biden, ambaye uamuzi wake ulikuwa umetangazwa na timu yake siku moja kabla.

"Wanajeshi wa Marekani na vikosi vilivyotumwa na washirika wetu wa NATO" watakuwa "wameondoka Afghanistan kabla ya maadhimisho ya miaka 20 ya mashambulio mabaya ya Septemba 11," ameszema rais wa Marekani.

Licha ya kuwepo kwa mpango huu wa wanajeshi wa Marekani kuondoka, kundi la Taliban limeendelea kushtumiwa kwa kushindwa kuacha mashambulizi dhidi ya serikali ya Afganistan lakini pia vikosi vya Marekani.