YEMENI

Muungano wa Saudia waharibu ndege tatu zisizokuwa na rubani Jazan

Mzozo wa Yemen unaowapambanisha waasi wa Kihouthi na serikali hauonyeshi dalili ya kumalizika, kulinganana wataaalamu.
Mzozo wa Yemen unaowapambanisha waasi wa Kihouthi na serikali hauonyeshi dalili ya kumalizika, kulinganana wataaalamu. STR AFP/File

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita nchini Yemen umeharibu ndege tatu zisizo na rubani zilizosheheni vilipuzi vilivyorushwa na waasi wa Houthi kuelekea mji wa kusini wa Saudi Arabia wa Jazan, televisheni ya serikali imeripoti leo Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Muungano huo umesema utachukua "hatua muhimu za kiutendaji" kulinda raia, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Muungano huo, ambao umeingilia kati kijeshi nchini Yemen tangu mwezi Machi 2015, mara nyingi umejibu mashambulio ya mpakani dhidi ya Saudi Arabia na mashambulio ya angani nchini Yemen.

Mzozo wa Yemen unaowapambanisha waasi wa Kihouthi na serikali hauonyeshi dalili ya kumalizika. Ikikabiliwa na vita, njaa na mapigano yasioisha, wataalamu wanasema ni vigumu kuirudisha nchi hiyo katika hali yake ya zamani.

Mwezi Machi tarehe 26 mwaka 2015 ndege za kivita za Saudi Arabia ziliingia kwenye anga ya Yemen na kuanza kushambulia ngome zote za wanamgambo  wa Kihouthi katika kile ambacho kilikuja kuwa ndio mwanzo wa mapigano makali ya kuwania udhibiti wa nchi hiyo masikini kabisa katika eneo la Mashariki ya kati.