AFGHANISTANI

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani azuru Kabul

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani (kulia) akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, huko Kabul, Afghanistan Aprili 15, 2021.
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani (kulia) akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, huko Kabul, Afghanistan Aprili 15, 2021. via REUTERS - Presidential Palace

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken yuko ziarani nchini Afghanistan tangu Alhamisi wiki hii, siku moja baada ya Joe Biden kutangaza kuwaondoa kabisa wanajeshi wa Marekani nchini  Afghanistan ifikapo Septemba 11, wizara ya mambo ya nje imebaini.

Matangazo ya kibiashara

Bw. Blinken, ambaye alihudhuria mkutano wa NATO huko Brussels Jumatano, amekutana na wanajeshi wa Marekani katika ubalozi wa Marekani na amezungumza na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.

"Niko hapa, hivi karibuni baada ya hotuba ya rais jana usiku (Jumatano), ili kuonyesha kweli, kwa uwepo wetu, kwamba tunaendelea na ushiriki wetu nchini Afghanistan," Antony Blinken amesema katika ubalozi wa Marekani huko Kabul.

"Ushirikiano huu unabadilika lakini unaendelea," ameongeza wakati wa mkutano wake na Ashraf Ghani katika ikulu ya rais.

Rais wa Afghanistan amesema anaheshimu uamuzi wa Washington na "kurekebisha vipaumbele vyake", kulingana na kundi la waandishi wa habari waliohudhuria mazungumzo ya wawili hao.