IRAN

Iran yaanza kurutubisha uranium kwa 60% Natanz

Iran imesema imeanza kurutubisha madini ya urani kwa asilimia 60, kiwango ambacho ni cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa baada ya hujuma iliyofanywa kwenye kinu chake cya nyuklia cha Natanz mwishoni mwa wiki iliyopita.
Iran imesema imeanza kurutubisha madini ya urani kwa asilimia 60, kiwango ambacho ni cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa baada ya hujuma iliyofanywa kwenye kinu chake cya nyuklia cha Natanz mwishoni mwa wiki iliyopita. HO Atomic Energy Organization of Iran/AFP/File

Iran imeanza kuzalisha madini ya uranium kwa asilimia 60 kwenye kinu chake cha nyuklia cha Natanz ambacho kilihujumiwa Jumapili ya wiki iliyopita, mkuu wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu Ali Akbar Salehi amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Tunazalisha karibu gramu tisa za uranium kwa 60% kwa saa," amesema Ali Akbar Salehi. "Lakini tunashughulikia mipango ya kupunguza uzalishaji hadi gramu tano kwa saa."

Spika wa bunge la Irani hapo awali alitangaza kwenye mtandao wa Twitter kwamba watafiti wa Iran wamefanikiwa kuanza kuzalisha asilimia 60 ya uranium.

Iran inabaini kwamba uamuzi wake wa kuzalisha uranium kwa asioimia 60 kama jibu kwa hujuma - ambayo inaiuhusisha Israeli dhidi ya kinu chake cha Natanz.