SYRIA

Syria kufanya uchaguzi wa urais nchini Mei 26

Rais wa Syria Bashar Al-Assad ambaye anawania katika uchaguzi wa Mei 26 muhula wa tatu.
Rais wa Syria Bashar Al-Assad ambaye anawania katika uchaguzi wa Mei 26 muhula wa tatu. ASSOCIATED PRESS - IBRAHIM USTA

Uchaguzi wa urais nchini Syria utafanyika Mei 26, bunge la nchi hiyo limetangaza Jumapili hii, uchaguzi ambao Rais Bashar al-Assad anatarajiwa kushinda muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Familia ya Rais Assad na Chama chake cha Baath wametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miongo mitano wakisaidiwa na idara za usalama zenye nguvu na jeshi viliopewa uwezo mkubwa wa kifedha na vifaa.

Utawala haumvumili mtu yoyote anayeukosoa. Mnamo mwaka wa 2011, ukandamizaji wa umwagaji damu ulitekelezwa na vikosi vya usalama vya Bashar al-Assaddhidi ya maandamano yanayounga mkono demokrasia uliiingiza Syria katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kulingana na sheria za uchaguzi, wagombea wanaotaka kuwania katika kinyang'anyiro hiki wanatakiwa wawe waliishi nchini Syria kwa miaka kumi kabla ya uchaguzi huo, hali ambayo inazuia wagombea wakuu wa upinzani wanaoishi uhamishoni.

Akikabiliwa na wapinzani wawili katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2014, Rais Assad alishinda kwa kura nyingi mno. Wapinzani wake walielezea uchaguzi kama mchezo wa uchaguzi.