YEMENI

Muungano wa Kiarabu wadai kuharibu ndege isiyokuwa na rubani ya waasi wa Houthi

Waasi wa Houthi wakiendelea na mapigano dhidi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.
Waasi wa Houthi wakiendelea na mapigano dhidi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia. REUTERS - KHALED ABDULLAH

Waasi wa Houthi wanaoshikilia sehemu kubwa nchini Yemen wamerusha ndege isiyokuwa na rubani kushambulia kambi ya jeshi katika mji wa Khamis Mushait, mji ulioko kusini mwa Saudi Arabia, msemaji wa kundi linalounga mkono Iran asema kwenye Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ulioingilia kati kijeshi nchini Yemen dhidi ya waasi wa Houthi umesema mifumo ya ulinzi wa anga ya Saudi Arabia ulinasa na kuharibu ndege isiyokuwa na rubaniya waasi wa Houthi.

Mzozo wa Yemen unaowapambanisha waasi wa Kihouthi na serikali hauonyeshi dalili ya kumalizika. Ikikabiliwa na vita, njaa na mapigano yasioisha, wataalamu wanasema ni vigumu kuirudisha nchi hiyo katika hali yake ya zamani.

Mwezi Machi tarehe 26 mwaka 2015 ndege za kivita za Saudi Arabia ziliingia kwenye anga ya Yemen na kuanza kushambulia ngome zote za wanamgambo  wa Kihouthi katika kile ambacho kilikuja kuwa ndio mwanzo wa mapigano makali ya kuwania udhibiti wa nchi hiyo masikini kabisa katika eneo la Mashariki ya kati.