ISRAELI

Israeli: Zaidi ya 40 wafariki dunia katika mkanyagano kwenye tamasha ya kidini

Watu kadhaa wafariki dunia katika mkanyagano Israeli katika tamasa la kidin, Aprili 30, 2021.
Watu kadhaa wafariki dunia katika mkanyagano Israeli katika tamasa la kidin, Aprili 30, 2021. REUTERS - JINI PHOTO AGENCY LTD

Mahujaji zaidi ya 40 wamepoteza maisha Kaskazini Mashariki mwa Israel baada ya kukanyagana wakiwa kwenye tamasha la kidini linalofahamika kama Lag B'Omer.

Matangazo ya kibiashara

Shirika linalohusika na majanga ya dharura nchini Israel hata hiyo halijasema idadi kamili ya watu waliopoteza maisha huku wengine wakiripotiwa kujeruhiwa.

Gazeti la Haaretz limeripoti kushuhudia miili ya watu 44, huku watu wengine 38 wakikimbizwa hospitalini kupata matibabu baada ya kujeruhiwa.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, tukio hilo ni msiba mkubwa na anawaombea wote waliojeruhiwa.

Walioponea mkanyagano huo wamesema, watu walianza kuangushana muda mfupi baada ya kuwepo kwa ujumbe wa dharura kuwa huenda kukatokea mlipuko wa bomu.

Picha na mikanda ya vídeo imewaonesha maelfu ya mahujaji wakiwa pamoja kabla ya kila mmoja kuanza kukimbilia usalama wake.

Tamasha la Lag Bomer, huadhimishwa kila mwaka na Wayahudi wenye dini ya Orthodox wanakusanyika kuwasha moto usiku kucha, wakiomba na kucheza.