AFGHANISTANI

Kabul yawekwa chini ya hali ya hatari

Askari wa Afghanistan amekaa nyuma ya gari la jeshi katika kituo cha ukaguzi nje kidogo ya mji wa Kabul, Afghanistan Aprili 21, 2021.
Askari wa Afghanistan amekaa nyuma ya gari la jeshi katika kituo cha ukaguzi nje kidogo ya mji wa Kabul, Afghanistan Aprili 21, 2021. REUTERS - MOHAMMAD ISMAIL

Usalama umeimarishwa Jumamosi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, ambayo inajiandaa kwa majambulizi yanayowezekana kutoka wanamgambo wa Taliban wakati wanajeshi wa Marekani bado wako Afghanistan kufuatia uamuzi wa rais Joe Biden.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza kwamba wanajeshi wa Marekani wataendelea kuepo nchini Afghanistan, kinyume na tarehe 1 Mei ambayo Donald Trump alikuwa alitangaza kuwa ndio tarehe ya mwisho kwa wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini Afghanistan.

Rais Joe Biden aliiweka tarehe Mosi Mei kuwa mwanzo rasmi wa kujiondoa kwa wanajeshi waliobakia nchini Afghanistan, lakini mchakato huo hautakamilika hadi tarehe 11 Septemba 2021, msimamo uliopingwa vikali na kundi la Taliban. 

Vituo vingi vya jeshi na vituo vya ukaguzi vimeonekana katika mji mkuu wa Afghanistan na chanzo ndani katika vikosi vya usalama kimesema mji huo umewekwa vhini ya hali ya hatari. Doria za kijeshi na usalama pia zimeongezwa katika miji mikubwa kote nchini, kulingana na chanzo hiki.

Wanajeshi wa Marekani walitarajiwa kuanza kuondoka Afghanistan Mei 1

Chini ya utawala wa rais wa Marekani Donald Trump, makubaliano yalifikiwa na Taliban mwezi Februari 2020, yakieleza kwamba wanajeshi wa kigeni wataanza kuondoka nchini Afghanistan ifikapo Mei 1, na Taliban itajizuia kushambulia vikosi vya jeshi na usalama na kambi za majeshi ya kigeni.

Lakini Rais Joe Biden alitangaza mwezi uliopita kwamba wanajeshi watasalia nchini kwa miezi kadhaa, huku makundi madogo madogo ya wanajeshi wa nchi hiyo wakiondoka nchini Afghanistan hadi Septemba 11.

Machafuko dhidi ya Waafghani yaliongezeka sana katika wiki za hivi karibuni, na kusababisha vifo zaidi ya 100 kati ya vikosi vya usalama vya Afghanistan.

Usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, mlipuko mkubwa ulisikika katika mkoa wa Logar mashariki mwa nchi na kusabbisha vifo vya watu kadhaa.