IRAQ

Makombora yarushwa katika uwanja wa ndege wa Baghdad, bila kusababisha hasara

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo makundi yenye silaha ambayo mamlaka nchini Iraq inayahusisha na Iran hapo zamani yalidai kuhusika na visa kama hivyo.
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo makundi yenye silaha ambayo mamlaka nchini Iraq inayahusisha na Iran hapo zamani yalidai kuhusika na visa kama hivyo. REUTERS - THAIER AL-SUDANI

Angalau roketi mbili zilianguka katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Baghdad, mji mkuu wa Iraq, jeshi la Iraq limesema, na kuongeza kuwa moja ya roketi hizo iliharibiwa na kudondoka karibu na uwanja wa ndege bila kusababisha hasara yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Hapo awali wawakilishi wa idara za usalama walisema roketi hizo lililolengwa katika shambulio la hapo awali, Aprili 22.

Hakuna akundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo makundi yenye silaha ambayo mamlaka nchini Iraq inayahusisha na Iran hapo zamani yalidai kuhusika na visa kama hivyo.

Kambi ya wanajeshi wa Marekani inapatikanakatika eneo hilo.