ISRAELI

Israel yatakiwa kusitisha ujenzi wa makazi mapya Mashariki mwa Jerusalem

Afisa wa polisi wa Israeli anazungumza na walowezi wa Kiyahudi nje ya nyumba walionyang'anya familia ya Wapalestina mwaka 2009, katika kitongoji cha Sheikh Jarrah Jerusalem Mashariki, Mei 6, 2021.
Afisa wa polisi wa Israeli anazungumza na walowezi wa Kiyahudi nje ya nyumba walionyang'anya familia ya Wapalestina mwaka 2009, katika kitongoji cha Sheikh Jarrah Jerusalem Mashariki, Mei 6, 2021. AFP - AHMAD GHARABLI

Umoja wa Mataifa unaitaka Israeli kuacha kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wanaoshi katika eneo la Mashariki mwa Jerusalem, hatua ambayo inasema itasababisha uhalifu wa kivita.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, inasema ardhi iliyochukuliwa na Israel, Mashariki mwa mji wa Jerusalem ni eneo la mamlaka ya Palestina.

Msemaji wa Tume hiyo Rupert Colville amesema kitendo kinachofanywa na Israel ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Onyo hili limekuja baada ya Wapalestina 15 kukamatwa katika sehemu hiyo ya ardhi  yenye mzozo walipokuwa wanaandamana kupinga kuondolewa katika ardhi hiyo yenye tata.

Mataifa ya Magharibi kama Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza yameitaka Israel kuachana na mpango huo