AUSTRIA

Tofauti kubwa bado zajitokeza kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia

Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Mambo ya Nje ya Ulaya (EEAS) Enrique Mora na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi wanasubiri kuanza kwa mkutano wa Kamati ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna, Austria, Mei 1, 2021
Naibu Katibu Mkuu wa Huduma ya Mambo ya Nje ya Ulaya (EEAS) Enrique Mora na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi wanasubiri kuanza kwa mkutano wa Kamati ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna, Austria, Mei 1, 2021 via REUTERS - EU DELEGATION IN VIENNA

Maafisa wa Marekani, Iran na Umoja wa Ulaya walisema Alhamisi wiki hii kwamba tofauti kubwa bado ipo kati ya Washington na Tehran kuhusu kurudi kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran wa 2015, ingawa afisa wa Marekani alisema makubaliano ndani ya wiki moja yanawezekana kama Iran itakuwa tayari.

Matangazo ya kibiashara

"Je! Inawezekana kuona pande zote mbili zinarudi kwenye mkataba wa nyuklia na kuuheshimu katika wiki zijazo, au makubaliano juu ya kuheshimiana? Ndio, inawezekana," afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema.

Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina lake katika mkutano wa kwa njia simu na waandishi wa habari, ameongeza kuwa "wanakimbizana na wakati" ikiwa dhana hii inawezekana. "Mwisho wa siku, uamuzi wa kisiasa ndio utachukuliwa nchini Iran."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Washington haina uhakika ikiwa Tehran iko tayari kufanya maamuzi muhimu kwa pande hizo mbili kurudi chini ya Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPoA) uliomalizika huko Vienna mwezi wa Julai 2015.

Mazungumzo kuendelea Vienna

Huko Tehran, mjadili mkuu wa nyuklia amesema bado kuna safari ndefu. "Kitakachotokea hakiwezekani kutabiri na ratiba haiwezi kupatikana," Abbas Araqchi ameiambia runinga ya serikali ya Iran.

"Iran inajaribu kufanikisha jambo hili haraka iwezekanavyo, lakini hatutafanya chochote kwa haraka," ameongeza.

Duru ya nne ya mazungumzo ya moja kwa moja itafungua Ijumaa huko Vienna kati ya maafisa wa Marekani na Iran, takriban miaka miwili baada ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuishutumu JCPOA na kurudisha vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.