ISRAELI-PALESTINA

Jerusalem: EU yatoa wito kwa Israeli kuchukua hatua haraka kwa komesha uhasama

Mwanamume huyu wa Kipalestina anasali, huku maafisa wa polisi wa Israeli wakikusanyika wakati wa makabiliano kwenye eno ambako kunapatikana Msikiti wa Al-Aqsa, unaojulikana kwa Waislamu kama eneo Tukufu, Jerusalem, Mei 7, 2021.
Mwanamume huyu wa Kipalestina anasali, huku maafisa wa polisi wa Israeli wakikusanyika wakati wa makabiliano kwenye eno ambako kunapatikana Msikiti wa Al-Aqsa, unaojulikana kwa Waislamu kama eneo Tukufu, Jerusalem, Mei 7, 2021. REUTERS - AMMAR AWAD

Umoja Ulaya umetoa wito kwa mamlaka ya Israeli kuchukua hatua "haraka" kwa "kuzuia" kuingezeka kwa mivutano huko Jerusalem, katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Mkuu wa sera ya nje na usalama wa Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 200 wamejeruhiwa mjini Jerusalem katika makabiliano makali kati ya wapalestina na vikosi vya usalama vya Israel.

Kulingana na shirika la hilali nyekundu ya Palestina, wengi wa waliopelekwa hospitali walikuwa na majeraha ya risasi za mpira. Polisi ya Israel imesema maafisa wake 17 walijeruhiwa katika makabiliano hayo.

Vurugu kati ya pande hizo mbili zimetokea katika maeneo matakatifu ya mji huo mkongwe na pia katika mji jirani wa Jarrah.

Maelfu ya waumini wa kiislamu walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo kwa salah ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kulingana na Polisi vurugu zilianza wakati maafisa wake waliporushiwa mawe kutoka upande wa Palestina.