ISRAEL-SIASA

Israeli: Vurugu Mashariki mwa Jerusalemu zatatiza uundwaji wa serikali mpya

Kijana wa Kipalestina anakabiliana na vikosi vya polisi Mashariki mwa Jerusalem, Mei 8, 2021.
Kijana wa Kipalestina anakabiliana na vikosi vya polisi Mashariki mwa Jerusalem, Mei 8, 2021. REUTERS - RONEN ZVULUN

Vurugu katika mji wa Jerusalem Mashariki, hasa kwenye Msikiti wa Alqsa, zinatishia kufanya hali kuwa ngumu kwa kambi inayopingana na Netanyahu kuunda serikali.

Matangazo ya kibiashara

Uchokozi dhidi ya sehemu hii takatifu na waumini waokuja kufanya ibada hapo haikubaliki. Nimstari mwekundu: onyo hili limetolewa na Mansour Abbas, kiongozi wa Ra'am, chama cha Kiisilamu. Katika hali ya kawaida, maneno haya hayangekuwa na athari yoyote. Lakini, na mgogoro wa kisiasawa sasa, maneno haya yana uzito mkubwa.

Bila uungwaji mkono wa wabunge wanne kutoka chama hicho kutoka kwa kundi la Muslim Brotherhood, Yair Lapid, mkuu wa chama cha mrengo wa kati, hana nafasi ya kuhamasisha walio wengi kumrithi Benjamin Netanyahu.

Vivyo hivyo, wabunge wengine ambao wanawakilisha  jamii ya walio wachache (21%) ya Waisraeli wenye asili ya Kiarabu wanaweza pia kuzuia kila kitu ikiwa makabiliano yataendelea.

Mshirika wake mkuu, Naftali Bennett, ni kiongozi wa chama kinachopigania makazi kamili kwa Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem. Kwa upande wake, Avigdor Lieberman, mzalendo mwingine, mwanachama wa muungano unaopambana na Netanyahu na ambaye ni mlowezi, anatetea hatua kali dhidi ya wale anaowaita "magaidi."  Hali ni nzito kwa uundwaji wa serikali ya walio wengi nchini Israel.