PALESTINA-ISRAEL

Makabiliano kati ya Wapalestina na vikosi vya Israel yaendelea

Kijanaa wa Kipalestina akiandamlana mbele ya askari wawili wa Israel huko Jerusalem Mei 7, 2021.
Kijanaa wa Kipalestina akiandamlana mbele ya askari wawili wa Israel huko Jerusalem Mei 7, 2021. AP - Maya Alleruzzo

Wapalestina kwa siku tatu wameendelea kukabiliana na maafisa wa Polisi wa Israel, wakati Israel ikiadhimisha siku ya mji wa Jerusalem, kama kumbukumbuku ya nchi hiyo kudhibiti maeno matakatifu ya mji huo mwaka 1967.

Matangazo ya kibiashara

Hali imekuwa hivyo katika êneo la msikitik wa Al-Aqsa, Mashariki mwa mji wa Jerusalem, wakati huu hali ya wasiwasi ikiendelea kushuhudiwa wakati huu Israeli inapopanga kuwaondoa kwa Wapalestina kwa nguvu katika Wilaya ya Sheikh Jarrah.

Mamia ya Wapalestina na polisi zaidi ya 20 wa Israel wamejeruhiwa, katika makabiliano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku tatu, sasa.

Wapalestina wanapinga kuondolewa katika êneo hilo, wanalosema ni ardhi yake , wakati huu kilio chão kikiuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameendelea kuwa serikali  itaendelea na mpango huo ili kuwapa maakaazi walowezi wa Kiyahudi katika êneo hilo, huku ikitetea uamuzi wake wa kukabiliana na waandamanaji wa Kipalestina.

Kesi kuhusu mzozo huo iliyotarajiwa kusikilizwa leo, imeahirishwa.