ISRAELI-PALESTINA

Mapigano yaendelea kurindima kati ya Waisraeli na Wapalestina

Wapalestina wakisafisha kiwanja cha msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem kufuatia mapigano mapya kati ya Wapalestina na polisi wa Israeli
Wapalestina wakisafisha kiwanja cha msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem kufuatia mapigano mapya kati ya Wapalestina na polisi wa Israeli Ahmad GHARABLI AFP

Wapalestina walirusha roketi kadhaa huko Israeli usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, wakati jeshi la Israeli limezindua mashambulio mapya ya angani kwenye Ukanda wa Gaza baada ya mapigano huko Jerusalem.

Matangazo ya kibiashara

Hasa, milipuko iliathiri majengo kadha katika Ukanda wa Gaza, na hali ya tahadhari ilishuhudiwa katika miji mingi kusini mwa Israeli.

Wapalestina wawili wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israeli, maafisa wa Palestina wameisema

Waisraeli sita wamejeruhiwa na roketi, madaktari wamesema.

Huko Gaza, Wapalestina ishirini, pamoja na watoto tisa, waliuawa katika mashambulio yaliyozinduliwa na Israeli Jumatatu baada ya mashambulio kadhaa ya roketi zilizorushwa na Wapalestina nchini Israeli. Roketi kadhaa ziliharibiwa na mfumo wa ulinzi wa makombora.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameshutumu makundi ya Wapalestina yenye silaha kwa "kuvuka mstari mwekundu" wakati Israeli ilisherehekea kumbukumbu ya kutekwa kwa mashariki mwa Jerusalem wakati wa Vita vya Siku Sita mwaka 1967 Jumatatu wiki hii. Mji wa Jerusalem ulikuwa haujalingwa kwa roketi tangu vita vya 2014 kati ya Israeli na Hamas.