ISRAELI-PALESTINA

Israel yaendelea na mashambulizi Gaza

Makabiliano kati ya vkos vya Israel na wapiganaji wa Hamas yasababisha uharibifu mkubwa, huko Gaza Mei 12, 2021.
Makabiliano kati ya vkos vya Israel na wapiganaji wa Hamas yasababisha uharibifu mkubwa, huko Gaza Mei 12, 2021. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Jeshi la Israel limeendelea kushambulia ngome za kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza, baada ya kundi hilo kurusha makombora kadhaa katika ardhi ya Israel. 

Matangazo ya kibiashara

Usiku wa kuelekea siku ya Jumatano, milio ya mashambulizi yamesikika katika eneo la ukanda wa Gaza huku kundi la kijihadi la Kipalestina la Kiislamu, likidai kurusha roketi zaidia ya 100 upande wa Israel.

Haya ndio mashambulizi makubwa uwahi kutekelezwa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza tangu mwaka 2014 wakati huu Waziri wa Israel akiapa jeshi lake litaendeleza mashambulizi zaidi.

Maafisa wa afya upande Pälestina, wanasema kuwa watu 35 wameuawa wakiwemo watoto 10 kufuatia mashambulizi ya wanajeshi wa  Israeli.

Jumuiya ya Kimataufa ikiongozwa na Umoja wa Mataifa na mataifa kama Maghairbi yameendelea kutoa wito wa kuwepo kwa utulivu.

Hali ilianza kuwa mbaya baada ya wiki iliyopita polisi wa Israel walipoanza kukabiliana na waandamanaji wa Kipalestina, nje ya msikiti wa Al-Aqsa, kupinga mpango wa Israeli kuwaondoa kwa nguvu Wapalesrina katika eneo la Sheikh Jarrah ili kutoa nafasi kwa walowezi wa Kiyahudi.