AFGHANISTAN

Taliban wafanya uvamizi dhidi ya wilaya iliyo karibu na Kabul

Visi vya jeshi vya Afghanistan huko Antonik katika mkoa wa Helmand.
Visi vya jeshi vya Afghanistan huko Antonik katika mkoa wa Helmand. - Afghanistan's Ministry of Defence office/AFP

Wapiganaji wa Taliban wanaidhibiti wilaya kutoka mikononi mwa vikosi vya serikali ya Afghanistan nje kidogo ya mji wa Kabul siku tatu kabla ya usitishaji vita kuanza, msemaji wa serikali amesema Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Wilaya ya Nerkh, karibu kilomita 40 kusini magharibi mwa mji mkuu, katika mkoa wa Wardak, ilitumika kwa miaka mingi kama mahali pa kuingia katika mhi wa Kabul au sehemu ya kuanzisha mashambulizi.

"Vikosi vya usalama na ulinzi vimejiondoa kama hatua ya kimkakati, katika makao makuu ya polisi katika wilaya ya Nerkh," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Tareq Arian ameliambia shirika la habari la AFP.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema waasi walichukua udhibiti wa wilaya hiyo Jumanne na waliteka makao makuu ya polisi na kituo cha jeshi.

Wizara ya Ulinzi ilisema Jumatano kwamba inatazamia kuzindua mashambulizi ili kuiweka tena chini ya himaya yake wilaya hiyo, ambapo watu zaidi ya 60,000 wanaishi. "Jeshi linajianda kuanzisha mashambulizi," amebaini Fawad Aman, msemaji wa Wizara ya Ulinzi.