PALESTINA-ISRAEL

Hakuna mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati Ijumaa

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa..
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.. Stephane LEMOUTON / POOL / AFP

Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliokuwa umepangwa kufanyika Ijumaa hii kujadili ghasia kati ya Israeli na Palestina hautafanyika, amesema msemaji wa uenyekiti wa baraza hilo linaloongozwa kwa sasa na China.

Matangazo ya kibiashara

 "Hakutakuwa na mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja w Mataifa Ijumaa wiki hii," msemaji huyo amesema Alhamisi wiki hii wakati wanadiplomasia kadhaa wananyooshea kidole cha lawama Marekani kwamba imepinga kikao hicho.

Hayo yanajiri wakati Hamas na Israel wameendelea kurushiana roketi na makombora ya angani, huku machafuko ya Wayahudi na Waarabu yakienea kote Israel.

Mzozo huo ambao umeingia siku yake ya nne leo haujaonyesha dalili za kupungua na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kampeni hiyo ya kuishambulia Gaza itachukua muda.