ISRAELI-PALESTINA

Israeli yaongeza mashambulizi yake ya anga Gaza, machafuko mapya yazuka

Moshi kwenye majengo ya Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa shambulio la anga la jeshi la Israeli, Mei 12, 2021.
Moshi kwenye majengo ya Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa shambulio la anga la jeshi la Israeli, Mei 12, 2021. AFP - SAID KHATIB

Mashambulizi kati ya Israeli na Palestina yameendelea usiku kucha kuamkia siku ya Alhamisi, katika machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu 65 wakiwemo watoto 14.

Matangazo ya kibiashara

Hivyo ndivyo hali ilivyo kati y apande zote mbili, wakati huu Israeli ikisema imewauwa Makamanda wakuu wa Hamas baada ya kushambulia jengo moja katika ukanda wa Gaza.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa iwapo hali hii haitasitihswa, huenda Israeli na Palestina zikaingia kwenye vita kamili.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema amezungumza na Waziri Mkuu wa Israel kuhusu kinachoendelea. 

Mpaka sasa haifahamiki ni lini makabiliano haya yataishi lini wakati huu Israel ikisisitiza kuwa itaendelea kulishambulia kundi la Hamas.

Machafuko haya yalianza wiki iliyopita baada ya Wapalestina kuanza maandamano kupinga kuondolewa kwa nguvu kutoka eneo wanalosema ni aradhi yao, Mashariki mwa mji wa Jerusalem.