ISRAELI-PALESTINA

Wapalestina 10 waangamia katika makabiliano na jeshi la Israeli

Polisi ya mipaka ikitoa ulinzi kwenye mtaa wa Jerusalem Mashariki wakati wa makabiliano na waandamanaji wenye hasira wa Palestina, Mei 14, 2021.
Polisi ya mipaka ikitoa ulinzi kwenye mtaa wa Jerusalem Mashariki wakati wa makabiliano na waandamanaji wenye hasira wa Palestina, Mei 14, 2021. REUTERS - AMMAR AWAD

Wapalestina kumi wameuawa Ijumaa wiki hii katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Walowezi katika makabiliano kadhaa na jeshi la Israeli, kando ya maandamano makubwa ya watu wenye hasira, kulingana na ripoti mpya kutoka wizara ya afya ya Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Wengi wa Wapalestina hawa waliuawa na risasi za moto na jeshi la Israel (IDF) katika maandamano ambayo yaliongezeka na kuwa makabiliano katika maeneo mbalimbali kote Ukingo wa Magharibi, wizara ya afya imeongeza, huku ikiripoti karibu majeruhi 150.

Wakati huo huo Israel imesema kuwa imepeleka ndege 160 za kivita katika Ukanda wa Gaza kuharibu mfumo wa njia za chini ya Ardhi unaoendeshwa na Hamas. Msemaji wa jeshi la Israel Kanali Jonathan Conricus amesema ingawa vifaru vinasaidiana na operesheni ya angani dhidi ya Ukanda wa Gaza, hakuna mwanajeshi wa Israel aliyeingia katika ukanda huo kama ilivyoripotiwa awali.

Watu wapatao 119 wameuawa Gaza na wengine wanane wameuawa Israeli tangu mapigano yalipoanza Jumatatu.

China yaishtumu Marekani katika usimamizi wake wa mzozo wa Israeli na Palestina

China imesema Marekani ingefikiria vema Palestina na mateso wanayopata Wapalestina. Haya ni majibu yake Washington kuzuia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati na dhidi ya ukosoaji wake kuhusu hali ya Waislamu katika Magharibi mwa China.