ISRAELI-PALESTINA

Israel yatekeleza mashambulizi mapya Gaza, zaidi ya vifo 200 vyaripotiwa

. Mamia ya majengo yameharibiwa, kulingana na serikali za mitaa, ambazo hazikuripoti majeruhi wowote. Jeshi la israel, Tsahal, limetete uamzi wake wa kutekeleza mashambulizi hayo likibaini kwamba yanalenga "ngome za magaidi" bila kutoa maelezo zaidi.
. Mamia ya majengo yameharibiwa, kulingana na serikali za mitaa, ambazo hazikuripoti majeruhi wowote. Jeshi la israel, Tsahal, limetete uamzi wake wa kutekeleza mashambulizi hayo likibaini kwamba yanalenga "ngome za magaidi" bila kutoa maelezo zaidi. AFP - ANAS BABA

Licha ya wito wa kusitisha uhasama, mapigano yanaendelea kwa siku ya saba mfululizo kati ya Israel na Palestina tangu mvutano kati ya Israeli na Hamas uanze tena. Zaidi ya vifo 200 vyaripotiwa kwa wiki moja.

Matangazo ya kibiashara

Usiku kucha wa Jumapili kuamkia Jumatatu, sawa na wiki moja sasa, Israeli inaendelea kurusha makombora katika Ukanda wa Gaza. Ndege za Israeli zimeshambulia Ukanda wa Gaza mara kadhaa kwa muda a dakika chache, na kusababisha umeme kukata. Mamia ya majengo yameharibiwa, kulingana na serikali za mitaa, ambazo hazikuripoti majeruhi wowote. Jeshi la israel, Tsahal, limetete uamzi wake wa kutekeleza mashambulizi hayo likibaini kwamba yanalenga "ngome za magaidi" bila kutoa maelezo zaidi.

Lakini wa Palestina, raia wanahofu kubwa ya kutokea maafa zaidi. "Hakujawahi kutokea mashambulizi makubwa kama haya," amesema Mad Abed Rabbo, 39, ambaye anaishi katika Jiji la Gaza magharibi. "Nilihisi kama ninakufa," alisema mkazi mwingine kabla ya kuongeza, "lazima Netanyahu atambue kwamba sisi ni raia, sio wanajeshi. "

Jumapili Jumuiya ya ushirikiano wa mataifa 57 ya Kiislamu ilikutana kwa dharura, kujadili mapigano makali yanayoendelea baina ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hamas linalodhibiti Ukanda wa Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa mamlaka ya Palestina Riad al-Malki, alilaani mashambulizi ya Israel aliyoyaita ya uoga wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, akiongeza kuwa uhalifu unafanywa dhidi ya Palestina bila ya kuwepo na athari.

Hata hivyo Mamlaka ya Palestina haina udhibiti dhidi ya kundi la Hamas na ukanda wa Gaza, ambako wapiganaji walichukua mamlaka mwaka 2007. Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Israel pekee ndio yenye kuwajibika na machafuko ya karibuni huko Jerusalem, Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.