PALESTINA-ISRAEL

Kamanda wa Islamic Jihad auawa katika shambulizi la Israeli Gaza

Uharibifu unaofanywa na jeshi la Israeli, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 17, 2021.
Uharibifu unaofanywa na jeshi la Israeli, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 17, 2021. REUTERS - STRINGER

Israeli imemuua kiongozi wa jeshi wa kundi la Islamic Jihad Jumatatu wiki hii katika moja ya mashambulizi yake ya anga huko Gaza, jeshi la Israel, IDF, na chanzo kutoka kundi la Islamic Jihad katika eneo la Palestina wameripoti.

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Houssam Abu Harbid, kamanda wa idara ya kaskazini ya Islamic Jihad, kinaweza kusababisha ulipizaji kisasi kutoka kwa kundi hilo kwani uhasama kati ya serikali ya Kiyahudi na wanaharakati wa Palestina huko Gaza umeingia wiki ya pili.

Katika taarifa iliyothibitisha kifo cha Houssam Abu Harbid, jeshi la Israeli linadai kwamba kamanda huyo wa Islamic Jihad "alihusika na mashambulizi kadhaa ya kigaidi dhidi ya raia wa Israeli."

Mashambulizi haya, kuanzia siku ya kwanza ya vita, yamejeruhi raia kadhaa nchini Israeli kulingana na jeshi la Israel, IDF.

Houssam Abu Harbid alikuwa kamanda wa Islamic Jihad kwa miaka 15, kulingana na IDF.