PALESTINA-ISRAEL

Misri yajaribu upatanishi na kufungua mipaka yake kwa majeruhi kutoka Gaza

Mamlaka ya Israeli inataka kulipiza kisasi kwa urusaji wa makomborokutoka Palestina dhidi ya Israel, wachambuzi wanasema.
Mamlaka ya Israeli inataka kulipiza kisasi kwa urusaji wa makomborokutoka Palestina dhidi ya Israel, wachambuzi wanasema. AFP - MAHMUD HAMS

Misri imeanza usuluhishi kati ya Israeli na Palestina wiki moja iliyopita. Upatanishi ambao, kwa sasa, haujafanikiwa. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana leo Jumatatu asubuhi, Mei 17 jijini Paris, na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kuunga mkono juhudi zake.

Matangazo ya kibiashara

Misri mwanzoni ilipendekeza mapatano ya saa 12 kati ya Wapalestina na Waisraeli. Usuluhishi huo utawezesha kufunguliwa kwa mazungumzo kati ya viongozi wa Hamas na maafisa wa Israeli.

Hali ambayo Cairo ilikuwa imefanikiwa kutumia wakati wa mizozo ya hapo awali kati ya Israeli na Hamas. Lakini ujumbe wa Misri ambao uliondoka kwenda Tel Aviv haukupokelewa na mamlaka ya Israeli, anaripoti mwandishi wetu huko Cairo, Alexandre Buccianti.

Mamlaka ya Israeli inataka kulipiza kisasi kwa urusaji wa makomborokutoka Palestina dhidi ya Israel, wachambuzi wanasema.

Ufaransa inataka "kusaidia upatanishi"

Ili "kuunga mkono usuluhishi wa Misri unaoendelea", Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sissi asubuhi ya Jumatatu hii, ameripoti mwandishi wetu Charlotte Cosset. Mazungumzo yao yamelenga hasa hali inayoendelea Mashariki ya Kati.

"Lengo la Ufaransa ni kukomesha ghasia zinazoendelea, kuunga mkono upatanishi wa Misri unaoendeleana kutoa wito wa pande zote kujizuia", Elysee ilisema.