ISRAELI-PALESTINA

Israeli na Hamas wakubaliana kusitisha mapigano Gaza

Wapalestina wanasherehekea makubaliano ya usitishaji vita katika mitaa mbalimbali huko Gaza, Mei 21, 2021.
Wapalestina wanasherehekea makubaliano ya usitishaji vita katika mitaa mbalimbali huko Gaza, Mei 21, 2021. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Israeli na Hamas kila upande umetangaza kwamba umekubaliana na suala la usiishwaji mapigano lenye lengo la kumaliza zaidi ya siku kumi za mapigano mabaya. Makubaliano hayo yalianza kutekelezwa Alhamisi, Mei 20 saa Tano usiku  za za Kimataifa sawa na saa 7:00 usiku za Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Israeli imebaini katika taarifa kwamba baraza la usalama "limekubali kwa kauli moja pendekezo la maafisa wote wa usalama kukubali mpango wa Misri wa kusitisha mapigano ya pande mbili." Hamas na Islamic Jihad, kundi la pili la wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha, wamebitisha kuanza kutekelezwa kwa makubaliano hayo saa 2 asubuhi Ijumaa (Alhamisi saa 5 usiku saa za kimataifa).

Hakuna roketi zilizofyatuliwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israeli, ambayo kwa upande wake hakifanya mashambulizi yoyotea ya angani katika eneo hilo.

Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia vilivyonukuliwa na shirika la habari la AFP, Misri inahusika na kuhakikisha kuwa usitishaji vita huu unaheshimishwa. "Wajumbe wawili kutoka Misri watatumwa kwenda Tel Aviv na maeneo ya Palestina kufuatilia utekelezaji wake na mchakato wa kudumisha hali thabiti kabisa," vyanzo hivyo vimesema.

"Ushindi" wa Hamas ?

Hamas imedai "ushindi" katika makabiliano yake ya silaha na Israeli, afisa mwandamizi wa kundi hilo amesema mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika Ijumaa kwa maandamano ya furaha katika Jiji la Gaza baada ya usitishaji wa vita kuanza.

Rais wa Marekani Joe Biden ameyakaribisha makubaliano hayo na ameeleza kuwa yanatoa nafasi muafaka kupiga hatua mbele baada ya siku 11 ya mashambulizi hatari, na kwamba amejitolea kwa hilo.

Punde tu muda wa kuanza utekelezaji wa makubaliano hayo ulipofika (saa nane usiku, majira ya Mashariki ya Kati), wakaazi wengi wa gaza walimiminika mitaani wakipaza sauti zao wakisema Mungu ni Mkubwa. Ishara ya afueni baada ya mashambulizi makali yaliyowanyima nafasi ya kusherehekea Siku kuu ya Idd El-Fitr wiki iliyopita.