ISRAELI-PALESTINA

Gaza: Umoja wa Mataifa waomba uheshimishwaji "kamili" wa usitishwaji mapigano

Watu 260 waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.
Watu 260 waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas. REUTERS - MOHAMMED SALEM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka pande lizokuwa zikihasimiana hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza (Israel na Hamas) kuheshimu kikamilifu usitishwaji mapigano. Hayo yamo katika tamko lake la kwanza la umoja huo tangu kuzuka kwa mzozo huo Mei 10.

Matangazo ya kibiashara

"Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa wamekaribisha tangazo la kusitisha mapigano la Mei 21 na wanatambua jukumu muhimu lililochukuliwa na Misri" na nchi zingine katika ukanda huo, imeongeza hati hiyo iliyoidhinishwa na Marekani baada ya kutolewa kwa kipengele kinacholaani machafuko.

Washington hadi sasa ilikuwa imekataa matamko matatu, na pia rasimu ya azimio la Ufaransa linalotaka "kusitishwa kwa uhasama mara moja" na kutaka "kutolewa kwa misaada ya kibinadamu bila kizuizi chochote kwa ukanda wa Gaza."

"Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataka usitishwaji mapigano" uweze kuheshimishwa, imebaini hati hiyo iliyopendekezwa na China, Norway na Tunisia, ambayo inabainisha tu kuwa nchi wanachama wa Baraza hilo "zinasikitishwa  na idadi kubwa ya raia kupoteza maisha katika mapigano hayo". Watu 260 waliuawa katika mapigano hayo.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "wamesisitiza kuhusu umuhimu wa kuwatolea haraka raia wa palestina misaada ya kibinadamu, hasa huko Gaza, na wameunga mkono mwito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa jamii ya kimataifa wa Kuijenga upya" Palestina, imeongeza nakala hiyo.