ISRAELI-PALESTINA

Marekani yaahidi kukarabati Ukanda wa Gaza

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ziarani Jerusalem Mei 25, 2021.
Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ziarani Jerusalem Mei 25, 2021. REUTERS - POOL

Marekani imeahidi kuimarisha uhusiano wake na Mamlaka ya Palestina kwa kufungua tena ubalozi wake mdogo Mashariki mwa Jerusalem na kusaidia katika ujenzi wa ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi ya jeshi la Israel.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema hayo baada ya kukutana na viongozi wa Palestina, huku akimhakikishia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa Marekani inaendelea kuunga mkono katika masuala ya usalama.

Waziri huyo wa Marekani amesema anatambua ugumu wa kurejesha hali ya kuaminiana kati ya Waisrael na Wapalestina baada ya mzozo wa wiki iliyopita.

Blinken amefanya mazunguzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na pia waziri wa mambo ya nje Gabi Ashkenazi na ameahidi kuwa Marekani itatoa mchango mkubwa katika kuukarabati Ukanda wa Gaza.

Ameongeza lakini kuwa Hamas haipaswi kufaidika kutokana na msaada huo.