MISRI-ISRAEL

Mikutano kati ya Israeli na Misri kuimarisha umoja Gaza yaendelea

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Aprili 13, 2021.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Aprili 13, 2021. DEBBIE HILL POOL/AFP/Archivos

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amempokea mkuu wa idara ya ujasusi wa Misri Jumapili hii na kumtuma waziri wake wa mambo ya nje Cairo kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kuimarisha amani kati ya Israeli na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Matangazo ya kibiashara

Misri imechangia katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa katika huko Palestina Mei 21 na tangu wakati huo imeratibu na Marekani na nchi zingine za ukanda huo kufikia makubaliano ya kudumu.

Benjamin Netanyahu, ambaye anashikilia siku zake za mwisho nafasi ya waziri mkuu, amesema mkutano wake na Abbas Kamel jijini Jerusalem umelenga usalama wa kikanda na jinsi ya kuwazuia wanamgambo wa Kiislam katika kundi la Hamas kupata misaada kwa ujenzi wa Ukanda wa Gaza, unaokadiriwa na mamlaka ya Palestina kwa makumi ya mamilioni ya euro.

Wasiwasi huu pia ulikuwa kiini cha ziara ya Gabi Ashkenazi jijini Cairo, mji mkuu wa Misri,  Jumapili hii kwa mazungumzo na mwenzake Sameh Choukry, ikiwa ni ziara ya kwanza kwa mwanadiplomasia wa Israeli katika mji mkuu wa Misri tangu miaka kumi na tatu iliyopita.