ISRAELI-SIASA

Isaac Herzog achaguliwa rais mpya na wa kumi na moja wa Israeli

Rais mpya wa Israeli Isaac Herzog (kushoto) na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Juni 2, 2021.
Rais mpya wa Israeli Isaac Herzog (kushoto) na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Juni 2, 2021. REUTERS - RONEN ZVULUN

Mwanasiasa wa muda mrefu Isaac Herzog kutoka chama cha Labour amechaguliwa kuwa rais wa Israeli, wadhifa mkubwa wa heshima. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikuwa wa kwanza kumpongeza.

Matangazo ya kibiashara

Isaac Herzog, anayejulikana pia kwa jina la maarufu "Mshumaa", anakuwa rais wa kumi na moja wa taifa la Israeli. Atachukua wadhifa wake baada ya mwezi mmoja tu, Julai 2.

Baba yake, Haïm Herzog, aliwahi kushikilia wadhifa huo. Isaac Hertzog amechaguliwa na wabunge wengi: 87 kati ya 120 wanaounda Bune la Knesset, dhidi ya mpinzani wake, mwanaharakati wa kijamii Miriam Peretz. Uchauzi ulifanyika kwa kura ya siri, ambayo ilikuwa muhimu kwa matokeo ya kura hiyo.

Rais mpya ni mwanasiasa mzoefu. Alitumia maisha yake yote ya kisiasa katika Chama cha Labour, ambacho alikuwa mwenyekiti. Hivi karibuni, aliongoza idara ya uhamiaji nchini Israeli. Wadhifa huu nchini Israeli ni wa kiishara, lakini unaweza kuwa na ushawishi mkubwa juu ya uteuzi wa mombea kwenye nafasi ya waziri mkuu. Na pia, kutoa msamaha wa rais au kuondoa hukumu.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea kutokota

Mazungumzo yamekwamisha serikali. Masuala kadhaa muhimu yameendelea kukosa majibu, hasa tume inayohusika na uteuzi wa majaji. Meno wa kulia na kushoto ndani ya muungano huu unaowezekana wanapingana vikali juu ya suala hili ambalo wanaamini ni muhimu. Kuna mizozo mingine kadhaa ambayo, kwa maoni ya wataalam, haiwezi kupatiwa suluhu. Kumesalia saa kumi ili kufikia suala hilo.

Usiku wa manane saa za Israeli mamlaka itarudi kwa Bunge la Knesset, ambayo haimaanishi kuwa juhudi za sasa za serikali hii ya mabadiliko zimeshindikana. Lakini hali hiyo itafanya mambo kuwa magumu zaidi na kuwapa wapinzani wa Naftali Bennett na Yaïr Lapid muda zaidi wa kujiandaa vizuri katika harakati zao.